Washitakiwa wa ghorofa, No dhamana

Haya tena lile sakata la gorofa lililoporomoka mnamo Juni 21 mwaka huu wakati likiendelea kujengwa, leo washitakiwa 6 leo wamepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kusomewa shitaka la kumsababishia kifo Bw. Shamte Said bila kukusudia.
 
Baada ya kuwasomea shitaka hilo, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo Charles Kenyela, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Sivangirwa Mwangesi, alisema washitakiwa waendelee kusota rupango bila dhamana kwani upelelezi bado haujakamilika.Pichani washitakiwa hao wakiwa ndani ya Mahakama wakisubiri kusikiliza kesi hiyo.
 
Kesi hiyo ya kuua mtu mmoja katika ajali hiyo ya kuporomoka ghorofa ambayo jana ni mara ya pili kufikishwa mahakamani hapo, ilisomwa na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Charles Kenyela mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Sivangilwa Mwagesi.
 
Ilidaiwa kuwa mnamo Juni 21, mwaka huu, washitakiwa walimuua Shamte Said Ganoga bila kukusudia baada ya jengo walilokuwa wakijenga katika Barabara ya Zanaki na Kisutu kuporomoka na kumsababishia kifo cha mtu huyo.
 
Kenyela alidai kuwa, kutokana na upelelezi wa polisi pamoja na daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marememu kutokamilika, aliiomba mahakama kutowapa dhamana washitakiwa.
 
Baada ya mwendesha mashitaka huyo kuomba ombi hilo la kuwanyima dhamana washitakiwa hao na mahakama kukubali, ndugu zao kadhaa waliokuwa ndani ya mahakama hiyo walianza kuangua kilio huku wakifuta machozi.
 
Kesi hiyo inayowakabili washitakiwa sita ambao ni Brown Undule, Jonas Mndeme, Athanas Mwageni, Kamtilal Premji, Satish Naran pamoja na Michael Mapunda itatajwa tena mahakamani hapo Julai 15, mwaka huu.
 
Washitakiwa wakiongea na Mawakili wao mara baada ya kesi hiyo yenye washitakiwa sita ambao ni Broun Undule, Jonas Mndeme, Athanas Mwageni, Kantilal Pemji, Satish Naran na Michael Mapunda itatajwa tena mahakamani hapo Julai 15 mwaka huu.